WAFAHAMU VIONGOZI WAPYA WA UNIONI MISHENI YA TANZANIA KUSINI YA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO 1. Mwenyekiti- Mch. Magulilo J Mwakalonge
Ametenda kazi kama mwinjilisti mlei, Mchungaji wa Mtaa (SWTF- SHC).
Mkurugenzi wa Uwakili- ETC, Mkurugenzi wa Mawasiliano - Tanzania Union,
Mkurugenzi wa Huduma na Katibu wa Chama cha Wachungaji - Tanzania Unioni
na kisha akishika nyadhifa hizo hizo katika Divisheni yetu ya ECD.
Kabla ya wito huu alikuwa Mkurugenzi wa Vijana, Muziki, na Chaplensia wa
ECD.
2. Katibu Mkuu- Mch James Machage- Ametenda Kazi Kama
mchungaji wa mtaa, Mkurugenzi wa Chaplensia wa Tanzania Union,
Mwenyekiti wa Mara Konference Kwa miaka karibia 15 na Katibu Mkuu wa
Mara Konferensi. Wakati akiitwa Mch Machage alikuwa Katibu Mwenza wa
Tanzania Union....
3.
Mhazini - Mr Jack Manongi- Ametenda Kazi Kama Mhasibu Mkuu wa Tanzania
Union kisha akijiunga na kitengo cha huduma za Ukaguzi cha general
Conference ambako ametenda kazi kama mkaguzi wa hesabu za fedha mpaka
wakati wa wito huu.
Tafadhali tuwaombee.
Tarehe 5-6
/12/ 2013 Wajumbe Kutoka makanisa yote ya Unioni Misheni ya Tanzania
Kusini watakutana Dar es salaam kuchagua kuchagua wakurugenzi wa unioni
hii. Tarehe 3-4/12/2013 Wajumbe toka Makanisa yote ya Unioni
Konferensi ya Tanzania Kaskazini watakutana Arusha kuchagua Viongozi na
Wakurugenzi wa Union hiyo. Tuendelee Kuombea zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment