Social Icons

Pages

Featured Posts

Tuesday, March 24, 2015

SIKU YA MATENDO YA HURUMA YAFANA KITUNDA KATI SDA

Ilikuwa siku ya kupendeza sana katika kanisa la Waadventista wa Sabato Kitunda Kati ambapo vijana walishiriki pamoja na vijana wenzo ulimwenguni kushiriki katika siku ya matendo ya huruma kama ilivyo utume wa kanisa hilo ulimwenguni . Zifuatazo ni picha za matukio mbali mbali katika siku hiyo:

                                         Kuwasili kwenye kituo cha DIANA ORPHANS


 

 
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wao na wageni waliowatembelea kutoka Kanisa la Waadventista wa Sabato Kitunda Kati

 
Miriam Chilwa akitumbuiza kuwafariji watoto yatima katika kituo hicho


Wakati wa kutoa kile walichokuwa nacho kwa ajili ya kusaidia watoto katika kituo hicho



 


Hatimaye wakati wa kurudi kanisani umewadia
 

Mungu awabariki  kwa kile mlichotoa

Wednesday, March 18, 2015

VIJANA KITUNDA KATI WAJIANDAA NA SIKU YA MATENDO YA HURUMA DUNIANI

Idara ya vijana kutoka kanisa la Waadventista wa Sabato Kitunda Kati wameendelea na maandalizi ya kushiriki katika siku ya matendo ya huruma ulimwenguni yatakayoendeshwa na chama hicho kushirikiana na Idara ya vijana, Sambamba na siku hiyo itafuatiwa na masomo ya vijana yatakayoendeshwa ulimwengu mzima kwa muda wa juma moja(wiki moja) , lengo ikiwa ni kuwajenga vijana kiroho, kiakili na kijamii hasa katika kipindi hiki cha siku za mwisho.



Kanisa la Kitunda Kati limepanga kuendesha masomo hayo kwa awamu mbili yaani saa 11 alfajiri na saa 11 jioni. ambapo saa 11 alfajiri itakuwa ni somo la vijana wa kati na vijana wakubwa, na jioni itakuwa ni somo kwa ajili ya vijana wadogo. Masomo hayo yataendeshwa na Samson Chiganga pamoja na Paul Misiwa ambao ni wakurugenzi wa chama cha watafuta njia katika mwaka huu 2015.
Tunapenda Kuwakaribisha wote kushiriki katika tukio hili  kubwa na la muhimu. Masomo yatatanguliwa na kwenda kuwaona watoto yatima tarehe 21/03/2015 kisha masomo yataendelea hadi tarehe 28/03/2015.
 Bwana awabariki mnapojiandaa kushiriki

Thursday, October 2, 2014

Watafuta Njia wa Kanisa la Kitunda Kati SDA wakiwa kwenye gwaride siku ya ufunguzi wa makambi ya mtaa wa Kitunda 2014

Watafuta njia (PF Club) wa Kitunda Kati SDA wakiwavisha wageni rasmi skafu wachungaji wageni ambao walitoa huduma kwenye kambi la mtaa wa kitunda

Mchungaji Sadik Lukinga akiwa na wageni wa kambi la mtaa wa Kitunda Kati

Kwaya ya CCB Kitunda Kati SDA wakitumbuiza kwenye kambi la mtaa wa Kitunda 2014

Makambi Mtaa wa Kitunda 2014

Waimbaji wa kwaya ya mtaa wa Kitunda wakitumbuiza kwenye makambi ya mtaa wa Kitunda 2014

Mass Choir iliyoundwa na kwaya ya Kitunda Kati SDA na Amani SDA wakijiandaa kuimba kwenye ibada kuu ya kambi la mtaa wa Kitunda 2014

Wednesday, August 6, 2014

KONGAMANO LA UIMBAJI KITUNDA AGOSTI 24, 2014

Kwaya ya CCB ya Kanisa la waadventista wasabato itakuwepo kwenye kongamano hilo


Kongamano kubwa la uimbaji wa kwaya za mtaa wa Kitunda.


Lini: Agosti 24, 2014 siku ya ufunguzi wa makambi ya mtaa wa Kitunda

WAPI: Kanisa la Waadventisa Wasabato Kitunda, Dar es Salaam

Muda: Kuanzia saa 4 asubuhi

Kwaya.  Kitunda SDA choir, Kitunda Kati SDA(CCB Choir) , Machimbo SDA Choir, Kiyombo SDA Choir, Ubungo SDA Choir na Majohe SDA Choir.

Pia kutakuwepo na kwaya za vijana za makanisa matano ya mtaa wa Kitunda

Kiingilio: Bureee

karibuni Wote