Kanisa la Kitunda Kati limepanga kuendesha masomo hayo kwa awamu mbili yaani saa 11 alfajiri na saa 11 jioni. ambapo saa 11 alfajiri itakuwa ni somo la vijana wa kati na vijana wakubwa, na jioni itakuwa ni somo kwa ajili ya vijana wadogo. Masomo hayo yataendeshwa na Samson Chiganga pamoja na Paul Misiwa ambao ni wakurugenzi wa chama cha watafuta njia katika mwaka huu 2015.
Tunapenda Kuwakaribisha wote kushiriki katika tukio hili kubwa na la muhimu. Masomo yatatanguliwa na kwenda kuwaona watoto yatima tarehe 21/03/2015 kisha masomo yataendelea hadi tarehe 28/03/2015.
Bwana awabariki mnapojiandaa kushiriki
No comments:
Post a Comment